Shambulio la Padri Charles Kitima,je nani anahusika?

DAR-Shambulio lililotokea kwa Padre Dkt. Charles Kitima limetikisa taifa, lakini pamoja na hisia kali zinazotolewa mitandaoni, kuna umuhimu mkubwa wa kulielewa tukio hili kwa kina na kuepuka hisia za kisiasa zisizo na ushahidi.
Kwa mujibu wa mashuhuda na wale waliowahi kufika katika makao makuu ya TEC pale Kurasini, eneo hilo lina ulinzi mkali sana, unaolindwa mithili ya "Ikulu ndogo."Si rahisi kabisa mtu asiye na uhusiano wa karibu kuvamia eneo hilo kiholela.

Kwa maelezo haya, hoja kuwa shambulio hilo lilitekelezwa na vyombo vya dola haina uzito wa kimantiki.

Kwani, kama lingekuwa tukio la kiusalama linaloendeshwa na mamlaka rasmi, je ni kwa nini lifanyike hadharani kwenye eneo linalojulikana kuwa na miundombinu madhubuti ya ulinzi?.

Zaidi ya hayo, taarifa zinaonesha kuwa mashambulizi hayo yalifanyika kwenye eneo la mgahawa-eneo ambalo si rahisi kwa mgeni asiye mwenyeji kuingia na kujichanganya bila kugundulika.

Hii inaonesha kuwa waliotekeleza hujuma hiyo walikuwa watu binafsi wenye ukaribu na padri, waliopanga kwa siri na kwa ustadi ili kujaribu kulifanya lionekane kuwa ni shinikizo kutoka juu.

Zaidi ya hapo, taarifa yenye ukakasi ni ile kwamba aliyetoa habari za kwanza ni Maria Sarungi, ambaye yupo nje ya nchi.

Hii inazua maswali ya msingi-alipataje taarifa kabla hata ya vyombo vya habari vya ndani, au hata familia ya karibu? Je, kuna ajenda ya kutengeneza mkanganyiko na kupotosha ukweli kwa manufaa ya kisiasa?.

Aidha, hoja ya PF-3 nayo inastahili kuangaliwa kwa makini. Ikiwa Padre Kitima alikimbizwa hospitali, je? Utaratibu wa kawaida wa polisi kupewa taarifa na fomu ya PF-3 ulifuatwa? Au ililenga zaidi kuzua taharuki kabla hata ya uchunguzi wa msingi?.

Na hata kama Padre Kitima alikuwa anakunywa kinywaji eneo la TEC, je? Hilo ni kosa? Hakuvunja sheria yoyote ya nchi, wala taratibu za kanisa. Eneo hilo ni makazi yake ya kazi na mapumziko, na analindwa kama raia mwingine yeyote.

Kwa hivyo, badala ya kuharakisha kutoa lawama kwa serikali au vyombo vya dola, tuchukue muda kusubiri uchunguzi wa kitaalamu unaoendelea kutoka kwa Jeshi la Polisi.

Wenye ajenda za kupindua ukweli kwa maslahi ya kisiasa ni muhimu wafichuliwe. Taifa halipaswi kuingizwa kwenye taharuki kwa misingi ya propaganda na hofu zisizo na msingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news