Wabunge waguswa na maboresho chanya Mahakama ya Tanzania

NA MARY GWERA
Mahakama

MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Twaha Mpembenwe amesema kuwa, maboresho ya Mahakama ya Tanzania yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika yana mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.
Hakimu Mkazi Mkuu na Mtaalamu Mchakata Taarifa, Mhe. Denice Mlashani (wa pili kushoto) akifafanua jambo kuhusu utendaji kazi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Mahakama mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti walipotembelea Ofisi hiyo leo tarehe 23 Mei, 2025.

Mhe. Mpembenwe ameyasema hayo leo tarehe 23 Mei, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma wakati wa Semina iliyotolewa kwa wajumbe (Wabunge) wa Kamati hiyo ya kujifunza kuhusu maboresho mbalimbali ya Mahakama nchini.

“Wakati mwingine mtu anaweza akafikiria kuwa, unaamua kesi mambo yanaisha hapana sisi kama Bunge, Kamati ya Bajeti tunaangalia sana ni jinsi gani kwa namna moja au nyingine Mahakama kama Mhimili unaojitegemea mbali ya kutoa haki kwa wananchi lakini vilevile unakwenda kuchochea katika suala zima la ukuaji wa uchumi na hiki ndicho kitu ambacho tumekuja kukiona kwa ukubwa zaidi,” amesema Mhe. Mpembenwe.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Twaha Mpembenwe akizungumza jambo leo tarehe 23 Mei, 2025 wakati wa Semina ya kujifunza maboresho ya Mahakama kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti ilipotembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiwasilisha mada kuhusu Maboresho ya Mahakama kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati kamati ilipotembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 23 Mei, 2025.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Dkt. Charles Kimei akichangia jambo.
Wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti pamoja baadhi ya watumishi wa Mahakama wakifuatilia wasilisho lililokuwa likitolewa na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel leo tarehe 23 Mei, 2025 katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini.
Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Kanda, Bw. Leonard Magacha (kushoto) akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti yeye pamoja na wenzake walipowasilisha katika viunga vya Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 23 Mei, 2025 kwa lengo la kujifunza maboresho ya Mahakama ya Tanzania.

Amesema kwamba, Kamati hiyo inaelewa kwamba mashauri yanaposikilizwa kwa wakati na haki inapokuwa imetendeka ina faida nyingi ikiwa ni pamoja na kuokoa muda ambapo amesema kuwa, muda ni sehemu muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Amesema kwamba, ana imani kuwa mbeleni zaidi, mashauri yatakavyoendelea kusikilizwa na kutolewa uamuzi kwa muda mfupi itaendelea kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi.

Ameongeza kwa kupongeza uongozi wa Mahakama ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu kwa maboresho ya miundombinu ya majengo ambayo Mahakama imejenga na inaendelea kujenga, huku akitoa mfano wa Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania kutumika kama kivutio cha utalii.

Amesema kuwa, Jengo la Makao makuu ya Mahakama ni utajiri katika nchi katika kuchochea uchumi kwa kuwa watu mbalimbali wanaokuja kujifunza wanachangia kukuza uchumi kupitia hoteli wanazofikia, chakula wanachokula na kadhalika.

“Napenda nikupongeze Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Ole na uongozi mzima kwa maboresho ambayo yanaendelea kufanyika ndani ya Mahakama, ni matarajio ya Kamati yetu na Bunge kwa ujumla kuona mambo makubwa na mazuri zaidi kuendelea kupatikana ndani ya Mhimili huu,” amesisitiza Mhe. Mpembenwe.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakioneshwa sehemu mbalimbali za Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania walipotembelea leo tarehe 23 Mei, 2025 kwa lengo la kujifunza maboresho ya Mahakama ya Tanzania.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya akifafanua jambo wakati wa semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti leo tarehe 23 Mei, 2025 katika Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti leo tarehe 23 Mei, 2025 katika Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma.

Amebainisha kuwa, kufuatia matunda mazuri ya Mahakama, waliona ni vema kuongeza bajeti ya Mhimili huo kwa mwaka ujao wa fedha 2025/2026 kiasi cha Tshs. 321 bilioni.

Akiwasilisha mada kuhusu Maboresho ya Miundombinu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel ameishukuru Kamati ya Bajeti na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano wa karibu ulioiwezesha Mahakama kupata mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongeza ufanisi katika shughuli za Mahakama kutokana na matumizi ya teknolojia.

Prof. Ole Gabriel amewaeleza Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa, Mahakama imefanikiwa kuanzisha mifumo mbalimbali ya TEHAMA ikiwemo Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Mashauri (JoT e-CMS); Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri Mwenendo wa Mashauri (TTS); Mfumo wa Takwimu (Data Hub); Mfumo wa taarifa za Hukumu na Sheria Tanzania (TAnzLII); na mingine.

“Kadhalika Mahakama imefanikiwa kuendelea kupunguza mrundikano wa mashauri mahakamani kutoka asilimia 10 mwaka 2020 hadi asilimia 4 mwaka 2025,” amesema Prof. Ole Gabriel.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakiwa katika Chumba cha Watoto na cha Kunyonyeshea walipotembelea Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania ili kujifunza kuhusu maboresho ya Mhimili huo.
Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya (kulia) akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti miundombinu ya TEHAMA iliyosimikwa katika moja ya chumba cha Mahakama kilichopo katika Jengo la Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania lililopo jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Dkt. Charles Kimei (kulia). Kushoto ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Eva Kiaki Nkya.

Ameongeza kuwa, Mhimili huo umefanikiwa pia kusogeza huduma karibu na wananachi kupitia ujenzi wa majengo na Mahakama zinazotembea sambamba na kuongezeka kwa imani ya wananchi kwa Mahakama asilimia 88 kulingana na utafiti uliofanywa na REPOA.

Aidha, Mtendaji Mkuu amewaeleza wajumbe wa Kamati hiyo kuwa, kwa siku za mbeleni Mhimili huo umejipanga kuanzisha utoaji huduma ya usikilizaji mashauri katika maji kupitia maboti, Mahakama zinazotembea na hata kwenye helikopta (Floating, Mobile & Flying Court).

Kadhalika amesema kuwa, Mahakam imejipanga kuharakisha utatuzi wa mashauri ya kawaida na mkakati wa kumaliza mashauri ya muda mrefu (Backlog); kuimarisha Ukaguzi na Usimamizi wa shughuli za Mahakama, kuendelea na ujenzi wa Mahakama.
Ukaguzi ukiendelea katika Jengo la Makao Makuu ya Mahakama.
Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mahakama ya Tanzania, Bw. Kalege Enock akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu namna Chumba cha Kusimamia na Kuratibu Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasilisho (TEHAMA) cha Mahakama kinavyofanya kazi.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Hawa Mnguruta akiwaeleza Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti namna Mfumo wa Unukuzi na Tafsiri (TTS) unavyofanya kazi wakati Wabunge hao walipotembelea Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma leo tarehe 23 Mei, 2025.
Picha ya pamoja kati ya Viongozi wa Mahakama na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti leo tarehe 23 Mei, 2025.(Picha na MARY GWERA, Mahakama-Dodoma).

“Tumejipanga pia kuendelea kutekeleza Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa Majengo ya Mahakama, kuboresha Mifumo na matumizi ya TEHAMA, kuongeza ushirikiano na wadau wa haki jinai na kuimarisha maendeleo ya rasilimaliwatu, mafunzo na nidhamu,” amesisitiza.

Kamati hiyo imetembelea na kuelimishwa kuhusu Chumba cha Kusimamia na Kuratibu Huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasilisho (TEHAMA) cha Mahakama ya Tanzania, Ofisi za Huduma kwa Mteja (Call Centre), Chumba cha Watoto na cha kunyonyeshea pamoja na ukumbi wa Mahakama (Court room).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news