SINGIDA-Kasi nzuri ya ukuaji wa uchumi nchini, ambayo imefikia asilimia 5.5 kwa mwaka, imechangiwa kwa kiasi kikubwa na bidii, juhudi na kujituma kwa wafanyakazi katika sekta mbalimbali.
Ukuaji huu umeiwezesha Serikali kufanya maamuzi muhimu ya kuboresha ustawi wa wafanyakazi, ikiwemo kupandisha kima cha chini cha mishahara kwa watumishi wa umma kwa asilimia 35.1.Hayo yalibainishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), yaliyofanyika kitaifa katika Viwanja vya Bombadia, mkoani Singida.

