Waziri Balozi Kombo awasili Geneva kusaka kura za Profesa Janabi

GENEVA-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amewasili Geneva katika kampeni ya kusaka kura za mgombea wa Tanzania Prof. Mohammed Janabi katika nafasi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Uwepo wake mjini hapo ni ishara na dhamira ya dhati ya kisiasa na mshikamano wa kitaifa, kwani anaungana na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jenista Mhagama, na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui, kuomba kura kwa Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika. Kwa pamoja, wanatoa wito wa kuunga mkono ombi la Rais Samia Suluhu Hassan la kumchagua kiongozi mwenye maono makubwa aliyejitolea kuboresha na kuimarisha ajenda ya afya barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news