DAR-Young Africans Sports Club imethibitisha kuwa Stephanie Aziz Ki raia wa Burkina Faso ameondoka klabuni hapo.
Aziz Ki anatajwa kuwa miongoni mwa vinara wa mabao katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambapo Wydad Casablanca imethibitisha kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili.
