DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaendelea kushiriki kikamilifu katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma kuanzia tarehe 16 hadi 23 Juni 2025.
Katika maadhimisho haya, wataalamu kutoka BoT wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuwekeza katika dhamana za Serikali, elimu kuhusu mikopo, pamoja na utambuzi wa alama za usalama zilizopo kwenye noti halali za Tanzania.