IRINGA-Wanamichezo zaidi ya 3,000 wanaoshiriki mashindano ya UMISSETA kitaifa mkoani Iringa wamepewa elimu kuhusu athari za dawa za kulevya.
Akizungumza wakati wa ufunguzi uliohudhuriwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwijuma, Afisa Elimu Jamii Mwandamizi wa DCEA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Queen Komba amesema, elimu hiyo inalenga kuwakinga vijana dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.
Ameongeza kuwa, matumizi ya dawa za kulevya huharibu afya ya akili, mwili, na nguvu kazi ya Taifa na Kutoa wito kwa vijana kuchukua hatua za makusudi kujiepusha na matumizi ya dawa hizo.
Mashindano ya UMISSETA mwaka huu yanajumuisha mikoa 28 na yanatarajiwa kufungwa Juni 29, 2025.
Tags
DCEA
DCEA Tanzania
Habari
Kataa Dawa za Kulevya na Timiza Ndoto Zako
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA)




