Huduma za NHC kivutio kwa wananchi Wiki ya Utumishi wa Umma 2025

DODOMA-Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma wameendelea kufurika katika banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) lililopo viwanja vya Chinangali Parks huku wengi wakitaka kufahamu taratibu za kupata nyumba bora na za kisasa zinazojengwa na shirika.
NHC ikiwa ni miongoni mwa taasisi na mashirika ya umma yanayoshiriki katika Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2025 yanayoendelea viwanjani hapo, maafisa wake wamekuwa wakitoa elimu ya kutosha kwa kila mwananchi anayefika katika banda hilo.

Maafisa hao akiwemo Mariam Chisumo na Ahmad Mwangu ambao ni maafisa Mauzo na Masoko wa NHC, pia wamewaeleza wananchi kuhusu miradi inayotekelezwa na shirika hilo jijini Dodoma.
Pia,wamewaeleza kuwa, NHC ina jukumu la kujenga nyumba za makazi na majengo mengine kwa ajili ya kuuza na kupangisha nchini.

Vilevile,shirika linajenga majengo kulingana na mipango iliyoidhinishwa na Serikali na juzalisha na kuwezesha uzalishaji wa vifaa vya ujenzi.

Jambo lingine ni kusimamia miliki za majengo yake na ya wamiliki wengine ikiwa ni pamoja na kuyafanyia matengenezo na kukusanya kodi za pango.
Sambamba na kuendesha shughuli za ushauri, upangaji na ukandarasi wa ujenzi wa nyumba na majengo.

Maadhimisho hayo yamefunguliwa leo Juni 17,2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.George Simbachawene ambapo yameanza Juni 16,2025 na yanatarajiwa kufikia tamati Juni 23,2025.
Mheshimiwa Simbachawene amepongeza wizara na taasisi za Serikali kwa kuweza kushiriki kwa wingi mwaka huu na kufanya maonesho hayo kufana huku akiwahimiza watumishi wa umma waendele kufanya kazi kwa bidii na weledi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news