NGARA-Leo Juni 10,2025 Kamati ya Pamoja ya Wataalamu ya Uimarishaji Mpaka wa Tanzania na Rwanda (JTC) imetembelea eneo la Mto Kagera lililopo wilayani Ngara mkoa wa Kagera ikiwa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa.
Eneo hilo la mto Kagera lililotembelewa ni sehemu ya mpaka wa kimataifa unaotenganisha nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi maarufu kama mafiga matatu pamoja na eneo la RUSUMO.

Lengo la kutembelea mpaka huo ni kuwezesha JTC Kuandaa mpango kazi wa uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili.
