DAR-Kocha wa Klabu ya Simba, Fadlu Davis ametozwa faini ya shilingi molioni mbili kwa kosa la kuishutumu Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kuwa ina ajenda tofauti kuhusiana na ratiba ya michezo ya klabu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Adhabu hiyo imetokewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) baada ya kocha huyo kuzungumza hayo kwenye mahojiano na Azam TV;