ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa katika Masjid Mushawwar, Mwembe Shauri, Mkoa wa Mjini Magharibi leo Juni 6,2025.
Mara baada ya Sala ya Ijumaa, Rais Dkt. Mwinyi alifika nyumbani kwa familia ya marehemu Sheikh Jabir bin Haydar bin Jabir Al-Farsy eneo la Kikwajuni, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi kutoa salamu za rambirambi pamoja na kuifariji familia hiyo kufuatia msiba wa Sheikh Jabir ulitokea tarehe 28 Mei 2025.













