ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na wananchi mbalimbali katika mazishi ya marehemu Abdallah Mohammed Bomba aliyefariki dunia jana.
Mapema, Alhaj Dkt. Mwinyi alishiriki sala ya maiti iliyofanyika katika Msikiti wa Mubarak Mazrui, Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Marehemu Abdallah Bomba amefariki jana wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Lumumba na amezikwa katika makaburi ya familia yao, Kwarara, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi.














