DAR-Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko makubwa ya uongozi serikalini kwa kuwahamisha na kuwateua viongozi mbalimbali wa mikoa, wilaya, wizara na taasisi za umma.

Wakuu wa Mikoa wapya: Balozi Simon Sirro (Kigoma), Mboni Mhita (Shinyanga), Beno Malisa (Mbeya), Kheri James (Iringa), na Jabir Makame (Songwe).
Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa: Kenan Kihongosi ahamishiwa Arusha; Anamringi Macha ahamishiwa Simiyu.
Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Mkuu: Agnes Meena (Wizara ya Mifugo), Dk. Hussein Omar (Elimu), Prof. Makenga na Mhandisi Kilundumya (mazingira na kilimo).
Makatibu Tawala wa Mikoa wapya: Abdul Mhinte (Dar es Salaam), Dk. Frank Hawasi (Songwe), pamoja na uhamisho wa wengine wawili kati ya Pwani na Tanga.
Wakuu wa Wilaya wapya: 17 wameteuliwa, akiwemo Mikaya Dalmia (Kigamboni), Thecla Mkuchika (Butiama), Benjamin Sitta (Iringa), na wengine.
Wakurugenzi wa Halmashauri: 12 wapya wameteuliwa, huku wengine wawili wakihamishwa.
Uteuzi wa Mkuu wa taasisi: Mhandisi Machibya Masanja kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC).
Uapisho wa viongozi walioteuliwa utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.