DAR-Kamati ya Utendaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ilikuwa na kikao kazi mjini Morogoro kuanzia Mei 21 hadi 23, 2025.
Ameeleza kuwa,katika kikao hicho kamati ilimteua ndugu William Shao, kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa TEF.
Pia, Kamati Tendaji imemteua Anita Mendoza aliyekuwa Kaimu Mtendaji Mkuu kuwa Mratibu wa TEF.
"Uteuzi huu ulianza Juni 1, 2025. Tunawapongeza Shao na Mendoza kwa kuteuliwa na tunawatakia mafanikio na utendaji mwema katika nafasi hizo."

