DAR-Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa, kuna mpango wa kuongeza kiwango cha chini cha mapato kinachotozwa kodi baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Kwa mujibu wa taarifa hizo za mitandaoni, kiwango cha chini cha mapato kitakachotozwa kodi kingepandishwa hadi shilingi 700,000.
TRA imetoa kanusho hilo leo Juni 11,2025, ikieleza kuwa, taarifa hizo ni za uongo na hazijatolewa na mamlaka hiyo;
