Tumieni fursa za miundombinu hii kuongeza uzalishaji katika kilimo-Rais Dkt.Samia

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi wa maeneo yanayozungukwa na Barabara ya Mzunguko wa Nje (Outer Ring Road) ya jijini Dodoma kutumia fursa za miundombinu hiyo katika kuongeza uzalishaji wa kilimo na uongezaji thamani wa mazao kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Muonekano wa Barabara ya Mzunguko ya Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3) jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.
Ametoa wito huo Juni 14,2025 wakati akizungumza na wananchi katika eneo la Nala mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo pamoja na mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato.

Rais Dkt. Samia amesema,kukamilika kwa miradi hiyo miwili mikubwa kutarahisisha usafirishaji wa mazao, pembejeo na bidhaa nyingine kwa gharama nafuu na kasi kubwa, hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa kuitumia kikamilifu kwa kuweka mipango madhubuti ya kuendeleza kilimo cha kisasa, hasa cha zabibu na alizeti ili kuongeza tija na kipato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja naRais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma(Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3) katika eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.
Aidha, Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa Serikali iliamua kuanzisha ujenzi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Dodoma yenye urefu wa kilomita 112.3 ili kukabili changamoto ya msongamano wa magari jijini Dodoma na kurahisisha biashara na usafirishaji kutoka Dar
es Salaam kuelekea Kanda ya Ziwa na nchi jirani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete maraa baada ya Kuwasili kugagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma(Dodoma outer ring road) yenye urefu wa km (112.3)katika eneo la Mtumba jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.

Akizungumzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, Rais Dkt. Samia amesema uwanja huo utakuwa lango jipya la kimataifa litakalosaidia kukuza biashara, utalii na nafasi
ya Dodoma kama makao makuu ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Nala jijini Dodoma mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato pamoja na ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa km (112.3) tarehe 14 Juni, 2025.
Katika hotuba yake, Rais Dkt. Samia pia ametoa shukrani maalum kwa Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, kwa ushirikiano na ufadhili uliotolewa na AfDB kwa miradi mbalimbali ya barabara nchini, ikiwemo ya Barabara ya Kabingo–Kasulu–Manyovu, Dodoma–Babati, Mnivata–Masasi, Sakina–Tengeru, ufadhili kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, pamoja na vipande viwili vya reli ya kisasa (SGR) inayounganisha Tanzania na nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakikagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025. ujenzi wa Kiwanja hicho cha Msalato unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na miundombinu mingine.
Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Rais Dkt. Samia amezielekeza Wizara
za Ujenzi na Uchukuzi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa na kwa ubora unaotakiwa, huku akisisitiza umuhimu wa kuitunza ipasavyo ili idumu kwa muda mrefu na kutoa tija iliyokusudiwa kwa Taifa.
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025. Ujenzi wa Kiwanja hicho cha Msalato unahusisha njia ya kuruka na kutua ndege (runway) jengo la abiria, jengo la kuongozea ndege pamoja na miundombinu mingine.
Katika kutambua mchango mkubwa wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika katika utekelezaji wa miradi hiyo na katika kuchangia maendeleo ya miundombinu nchini Tanzania, Rais Dkt. Samia ameridhia pendekezo la Wizara ya Ujenzi la kuipa jina barabara hiyo ya mzunguko wa nje wa Dodoma la “Barabara ya Dkt. Akinwumi Adesina.”
Matukio mbalimbali kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Nala jijini Dodoma tarehe 14 Juni, 2025.
Akiwa nchini, Dkt. Adesina alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sayansi (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutokana na mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya Bara la Afrika kupitia sera za fedha na programu bunifu za maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news