Waziri Mkuu aagana na Balozi wa Angola aliyemaliza muda wake nchini

■Ampongeza kwa kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini

■Balozi de Oliveira asema Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania

DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 28, 2025 amemuaga rasmi Balozi wa Angola nchini Tanzania, Sandro Agostinho de Oliveira, ambaye anamaliza muda wake wa uwakilishi baada ya kutumikia nchi yake kwa mafanikio makubwa ya kidiplomasia nchini.Mheshimiwa Majaliwa ambaye ameagana na Balozi huyo jijini Dodoma kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu, amempongeza Balozi de Oliveira kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kisiasa na kijamii kati ya Tanzania na Angola.
Mheshimiwa Majaliwa amemweleza balozi huyo kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuthamini na kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia na kidugu kati ya Tanzania na Angola katika nyanja zote muhimu za maendeleo.
Balozi de Oliveira ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote wa uwakilishi wake na amesema kuwa Angola itaendelea kuwa mshirika wa karibu wa Tanzania katika kuendeleza ustawi wa nchi hizo mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news