DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Juni 24, 2025 amezindua mitambo ya uchorongaji na vifaa vya utafiti kwa wachimbaji wadogo kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma.





