DAR-Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na Kenya Airways (KQ) leo imetia saini makubaliano ya kwanza ya aina yake ya kushirikiana katika kubadilishana ujuzi wa kiufundi kuhusu uendeshaji, huduma za mizigo na kuimarisha ubora wa huduma za pamoja.

Makubaliano haya yanalenga kujenga uwezo wa ndani kwa vitendo na kuimarisha mashirika yetu kwa maendeleo endelevu ya sekta ya usafiri wa anga barani Afrika.