DAR-Wanafunzi kutoka shule mbalimbali jijini Dar es Salaam wametembelea banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kuanzia tarehe 28 Juni hadi 14 Julai 2025.
Miongoni mwa shule zilizoshiriki ni Shule ya Msingi Gilman Rutihinda, Shule ya Sekondari Tusiime, na Shule ya Seminari ya Kisarawe. Wanafunzi kutoka shule hizo walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo kuhusu majukumu na shughuli mbalimbali za Benki Kuu.
Pia, walielimishwa kuhusu alama za usalama zinazopatikana katika noti halali za Tanzania pamoja na njia sahihi za utunzaji wa noti hizo.



