CCM kuteua wagombea ubunge na udiwani Julai 28,2025

DODOMA-Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) itafanya kikao chake cha kawaida Julai 26, 2025 tofauti na matarajio ya awali kuwa kingefanyika Julai 18 au 19,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 19, katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amesema kikao hicho cha NEC kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC), ambacho pia kitafanyika siku hiyo hiyo ya Julai 26,2025.

Makalla amesema maandalizi ya vikao hivyo yanaendelea vizuri, huku akibainisha kuwa hatua hizo ni sehemu ya mchakato wa uchaguzi ndani ya chama unaoendelea kwa mujibu wa ratiba rasmi.

Aidha, ameeleza kuwa Julai 28, 2025, Kamati Kuu ya CCM itakutana tena kwa ajili ya kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa ubunge na wajumbe wa baraza la wawakilishi kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni kwa ratiba itakayopangwa baadaye.

"Wagombea ni wengi sana, kwa hiyo kazi ya kuchambua ni kubwa na sisi tunataka tutende haki na tuifanye kwa umakini. Kwa hiyo uteuzi wa mwisho utafanyika tarehe 28 na baada ya hapo kwenda kwenye kura za maoni."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news