Mabondia wa Tanzania watwaa makombe Comoro

MORONI-Mabondia Kassim Mbundwike na Mwanjango wameshinda mapambano yao katika michuano ya maadhimisho ya miaka 50 ya Sherehe za Uhuru wa Umoja wa Visiwa vya Comoro iliyoshirikisha mabondia toka Madagascar, Gabon, Tanzania na wenyeji Comoro.
Mabondia hao wamewasilisha vikombe vyao kwa Balozi wa Tanzania nchini humo,Saidi Yakubu kwa uratibu wa mwambata jeshi,Abdulrahim Mahmoud Abdallah.
Balozi Yakubu aliwapongeza kwa ushindi huo ambao umefungua ukurasa mpya wa diplomasia ya michezo.Michuano hiyo ilihudhuriwa na Rais wa Umoja wa Visiwa hivyo,Azali Assoumani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news