MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imewataka wananchi wote wanaomiliki au kutumia ndege nyuki (drone) kuhakikisha wanazisajili ili kulinda usalama wa anga na kuzingatia sheria.
Akizungumza kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) Sabasaba, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Salim Msangi, amesema usajili wa drone ni lazima na si hiari kwani zikitumika vibaya zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa.
"Drone zinapaswa kusajiliwa kama ndege nyingine na zikitumika kiholela zinaweza kutumika kama silaha au kwa shughuli zisizo salama. Ndio maana tunasisitiza zisitumike bila kibali kutoka TCAA," amesema Msangi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)






