DODOMA-Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa Kikao cha Kawaida cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitafanyika Jumamosi, Julai 19, 2025 saa 4:00 asubuhi, katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM, jijini Dodoma.Kikao hicho kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, na Rais Samia Suluhu Hassan.


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Itikadi, Uenezi na Mafunzo), CPA Amos Gabriel Makalla, amesema kwenye taarifa kuwa kikao hicho kinatanguliwa na vikao vya Sekretarieti ya CCM Taifa vinavyoendelea jijini Dodoma kwa ajili ya kupokea na kuchambua majina ya wagombea wa Ubunge na Baraza la Wawakilishi, majimbo na viti maalum.
Kikao cha Jumamosi kinatarajiwa kujadili ajenda mbalimbali muhimu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





















