MKUU wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi mstaafu, Simon Sirro amesema pato la Mkoa limeongezeka kutoka Sh trilioni 4.1 mwaka 2020 hadi Sh trilioni 5.6 mwaka 2024, sawa na ukuaji wa asilimia 38.6, ikiwa ni matokeo ya jitihada za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, pato la mwananchi Kigoma limepanda kutoka milioni 1.4 hadi milioni 2.1 katika kipindi hicho, sawa na ongezeko la asilimia 45.4.Ameyasema hayo Julai 19,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafanikio ya miaka minne ya serikali ya awamu ya sita
Sirro amesema, Kigoma ina fursa nyingi za uwekezaji kutokana na jiografia ya kipekee, ardhi yenye rutuba, vivutio vya utalii na uwepo wa Ziwa Tanganyika.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo














