Magazeti leo Julai 30,2025

CHAMA a Mapinduzi (CCM) kimetangaza uteuzi wa awali wa wagombea wa nafasi za ubunge kwa majimbo yote 272 ya Tanzania Bara na Visiwani. Katika mchakato huo, jumla ya wagombea zaidi ya 5,000 wamejitokeza kuwania ubunge huku zaidi ya 30,000 wakichukua fomu kuwania nafasi za udiwani.
Taarifa hiyo imetolewa Julai 29, 2025 jijini Dodoma na CPA Amos Makalla, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Chama hicho ( White House) , CPA Amos Makalla amesema uteuzi huo umefanywa kwa kuzingatia sifa, uwezo wa mgombea, na mahitaji ya kisiasa ya majimbo husika.

‎Chama pia kimetoa wito kwa wale ambao hawakupata nafasi kwa sasa kutokata tamaa, bali waendelee kukiunga mkono CCM kwani nafasi za kulitumikia chama bado ni nyingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news