Mataifa 25 yenye vikosi bora vya majeshi duniani

 Jarida la Kimataifa la Firepower ambalo huwa linalinganisha uwezo wa vikosi vya majeshi duniani kila mwaka, limetoa orodha ya mataifa 138 pamoja nguvu walizonazo, Mwandishi Diramakini anakusogezea orodha ya mataifa ya 25 bora kwa uwezo wa kijeshi.

Hii ni baada ya ripoti hiyo kuangalia idadi ya silaha, jeshi na rasilimali fedha ambazo nchi hizi hutumia katika operesheni za kijeshi katika maeneo mbalimbali.

Aidha, nafasi ya kwanza katika orodha huwa haibadiliki kila mwaka, lakini baadhi ya nchi huwa zina uwezo tofauti kila mwaka kulingana na jarida hilo, zifuatazo ni nchi na nafasi yake katika orodha;

1: Marekani, 2:Urusi,3:China, 4:India,5:Japan,6:Korea Kusini, 7:Ufaransa,8:Uingereza, 9:Misri, 10:Brazil,11:Uturuki, 12:Italia, 13:Ujerumani,14:Iran,15:Pakistan, 16: Indonesia, 17: Saudi Arabia,18:Israel, 19: Australia, 20:Hispania,21: Poland, 22:Vietnam, 23:Thailand, 24:Canada na 25:Korea Kaskazini.

Hata hivyo, kwa mujibu wa jarida hilo, baadhi ya Mataifa yameshuka viwango kidogo wakati mengine yakiwa hayana ongezeko lolote katika nafasi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

Previous Post Next Post

International news