DAR-Naibu Gavana mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Juma Reli ameipongeza BoT kwa juhudi zake katika kusimamia maendeleo ya uchumi wa nchi, kuimarisha sekta ya fedha, kuboresha mifumo ya malipo, pamoja na kuendeleza huduma jumuishi za fedha kwa wananchi.

Bw. Reli ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake katika banda la Benki Kuu kwenye Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Alieleza kuwa hatua na mikakati mbalimbali ya Benki Kuu imeendelea kuchochea ustawi wa uchumi na kuongeza ushirikishwaji wa wananchi wengi zaidi katika huduma za fedha.





