DODOMA-Kamati Kuu ya Halmashauri ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa,katika kikao chake kilichofanyika tarehe 28 Julai, 2025 jijini Dodoma, pamoja na mambo mengine, imepitia na kujadili majina ya wanachama wake walioomba kupendekezwa katika mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM.































































