ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt.Hussein Ali Mwinyi amefanya uteuzi na mabadiliko ya vituo vya kazi kwa wakuu wa mikoa na wilaya kama ifuatavyo:

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.
1. Mheshimiwa Hamida Mussa Khamis ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja.
2. Mheshimiwa Cassian Gallos Nyimbo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "A" Unguja.
3. Ndugu Rajab Ali Rajab ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati Unguja.
4. Ndugu Miza Hassan Faki ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba.
5. Ndugu Mohammed Ali Abdallah ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja.
6. Ndugu Amour Yussuf Mmanga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "B", Unguja.
