Shilingi Bilioni 67.507 kuimarisha elimu ya sekondari mikoa ya Pwani na Lindi

LINDI-Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kupitia Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) katika Mkoa wa Lindi imetoa Shilingi Bilioni 31.72 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya shule ikiwemo ujenzi wa shule mpya za sekondari za kata 28.
Fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule 1 ya Bweni ya Wasichana ya Mkoa, ujenzi wa shule ya 1 ya bweni ya Wavulana ya kanda, ujenzi wa shule 1 ya Amali ya Mkoa, ujenzi wa Shule 3 za Amali za Wilaya, ujenzi wa nyumba 18 za walimu, ujenzi wa mabweni 11, madarasa 18 na matundu ya vyoo 52 katika shule za Sekondari.
Pia, kupitia programu hiyo ya SEQUIP serikali imetoa Shilingi Bilioni 35.791 katika mkoa wa Pwani ambazo zimetumika kukarabati shule kongwe, kujenga shule mpya za kata, shule ya Wasichana, shule ya kanda ya wavulana, mabweni, madarasa na matundu ya vyoo katika shule za Sekondari.

Vilevile katika utekelezaji wa mradi huo serikali imejenga nyumba za walimu katika shule 12 za kata za awamu ya kwanza (2 in1), ujenzi wa bweni, ukarabati wa maboma ya madarasa, ukarabati wa maboma ya maabara na ukarabati wa maboma ya matundu ya vyoo.
Pia,fedha hizo zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa shule 11 za sekondari za kata, shule 2 za Amali za kitaifa zilizopo Rufiji na Chalinze, na ujenzi wa shule 4 za amali za kawaida awamu ya kwanza. Vilevile upanuzi wa shule za sekondari ziwe za kidato cha tano, na kuongeza mabweni, Ujenzi wa madarasa 30, mabweni 25 na matundu ya vyoo 116 kwenye shule 12 za sekondari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news