DAR-Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga SC,Ally Kamwe amesema,Stephanie Aziz Ki anatarajiwa kurejea klabuni hapo.
Ni kutokea klabu ya Wydad Casablanca baada ya kumaliza mkataba,kwani makubaliano yao ilikuwa ni kuwatumikia Wydad kwa mkataba wa miezi mitatu.

Kamwe ameeleza kuwa,kwa mujibu wa makubaliano ilikuwa hadi kufikia Julai 10,mwaka huu Wydad wawe wameshawasiliana na Yanga SC.
"Kama Wydad watakuwa wanaongeza maana yake wamalizie kiasi ambacho tulikubaliana ila kama watasema arudi sawa arudi aje awashone maana bado amebaki na mwaka mmoja."