IRINGA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 05, 2025 ameshiriki katika mbio za Great Ruaha Marathon (GRUMA 2025) zilizoanzia na kuishia kwenye eneo la Ibuguziwa, ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Lengo la Mbio hizo ni kuhamasisha uhifadhi wa mazingira wa Mto Ruaha Mkuu ambao ni uti wa mgongo wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuifanya jamii kuona umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuhimiza matumizi endelevu ya rasilimali za asili.