Dkt.Abbas aitaka Kamati ya Ukaguzi iwe jicho la Wizara ya Maliasili

DAR-Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas amezindua Kamati ya Ukaguzi ya wizara hiyo, huku akiitaka kuwa jicho la wizara katika kupunguza hoja za ukaguzi, kukabiliana na majanga, na kuifanya sekta ya Maliasili na Utalii iendelee kutoa mchango wake kwenye pato la Taifa.
Kamati hiyo itakayohudumu kwa kipindi cha miaka mitatu inaongozwa na Idrisa Mohamed kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania kama Mwenyekiti, huku wajumbe wakiwa ni Emmanuel Kihampa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Mark Chuwa kutoka Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania, Dkt. Tuli Msuya kutoka Mfuko wa Misitu na Bruno Melikiori kutoka Wizara ya Ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news