Rais wa Simba Sc na Mwenyekiti wa Bodi, Mohammed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba SC huku yeye akiendelea kubaki kama Mwekezaji na Rais wa Wekundu hao wa Msimbazi. 

Mo Dewji ametangaza uamuzi huo Septemba 04, 2025 hatua inayokuja kutokana na majukumu yake mengine na ukweli kwamba mara nyingi yupo mbali hali iliyopelekea kuona klabu hiyo inahitaji kiongozi wa bodi ambaye yupo karibu, mwenye muda wa kutosha na anaweza kushiriki kwa ukaribu zaidi katika shughuli za kila siku.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















