ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi usiku wa Septemba 4,2025 amejumuika na waumini wa Kiislamu katika Maulid Makuu ya Kitaifa ya Kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika Mnazi Mmoja.
Maadhimisho hayo yametimiza miaka 99 tangu kuanzishwa mwaka 1926, yakihusisha wananchi na waumini kutoka sehemu mbalimbali za Zanzibar.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Mama Mariam Mwinyi, pamoja na viongozi wa dini.

















