ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na ujumbe wa Jukwaa la Mabunge ya Nchi Wanachama wa Sekretarieti ya Ukanda wa Maziwa Makuu (FP-ICGLR) Ikulu, Zanzibar.

FP-ICGLR ni miongoni mwa misheni zitakazopeleka waangalizi katika mikoa yote ya Zanzibar kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28 na 29, 2025.



















