Waziri Kombo apokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Uholanzi

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amepokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ufalme wa Uholanzi Mheshimiwa Marjo Johanna Jacoba Crompvoets, katika hafla iliyofanyika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Mhe. Kombo amempongeza Mheshimiwa Crompvoets kwa uteuzi wake na amemuhakikishia ushirikiano wakati wote atakapokuwa anahudumu hapa nchini.
Aidha,Waziri Kombo ameipongeza Serikali ya Uholanzi kwa jitihada za kuanzisha miradi mbalimbali inayoigusa jamii moja kwa moja na kuleta maendeleo ya jamii ikiwemo katika sekta za miundombinu, elimu, afya, mifugo, biashara na uwekezaji na utalii.

Naye Mhe. Crompvoets ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano uliopo na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kupitia maeneo ya kipaumbele yakiwemo kilimo cha mbogamboga, matunda na maua.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news