SERIKALI imetangaza washitakiwa 1,736 kati ya 2,045 waliokamatwa na kushitakiwa kwa makosa ya kula njama na uhaini kutokana na vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu, wataachiwa. 

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.Juma Homera ametangaza hayo katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Njedengwa mkoani Dodoma. Dk Homera amesema Novemba 18, mwaka huu Rais Samia alitoa msamaha kwa walioshiriki maandamano kwa kujua au kutokujua na kwa mujibu wa takwimu alizozitoa ni kuwa kulikuwa na jumla ya waandamanaji 2,045 walikamatwa nchi nzima kutokana na tukio hilo.
Amesema kutokana na maelezo ya Rais Samia watakaoachiwa kwa sasa ni 1,736 na hadi Novemba 25, mwaka huu walikuwa wameachiwa 607 na bado wanaendelea kuwaachia baada ya upekuzi wa kina na kujiridhisha ili waweze kutoka.“Na zoezi linaendelea lakini katika hao 2,045 watu 309 kazi ya ufuatiliaji bado inaendelea lakini kwa kweli watakaoachiwa ni 1,736 kati ya hao na walioachiwa hadi tarehe 25 ni watu 607,” alisemaa Dkt.Homera.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















