Magazeti leo Desemba 23,2025

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ametoa wito kwa wazaliwa wa Mkoa wa Kagera waliopo maeneo mbalimbali duniani kuhakikisha wanalea watoto wao kwa maadili na kuwafundisha utamaduni wa mkoa huo.
Amesema hayo katika kilele cha Tamasha la Ijuka Omuka msimu wa tatu mwaka 2025, lenye kaulimbiu ya ‘Wekeza Kagera Irudishe Katika Ubora’, ambalo lilipambwa kwa maonesho mbalimbali ya utamaduni, vyakula vya asili, ngoma za asili na historia za makabila mbalimbali ya Kagera.
Baadhi ya viongozi wengine walioshiriki tamasha hilo ni Naibu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Julieth Kabyemela, Mkuu wa Mkoa wa Kagera,Fatma Mwassa.

Waliohudhuria walipata chakula cha asili, walipokea simulizi na wengine kupata mavazi mbalimbali yanayotambulisha Mkoa wa Kagera.

Waziri Simbachawene alisema amevutiwa na historia na utamaduni wa Mkoa wa Kagera na kusema kama wazazi hawatashiriki kikamilifu kuwarithisha watototo wao utapotea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news