Taarifa muhimu kutoka Jeshi la Polisi Tanzania leo Desemba 9,2025


Jeshi la Polisi lingependa kueleza kuwa, kuna hii picha mjongeo ya zamani na nyinginezo zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikihadaa wananchi kuwa maandamano yameshaanza.

Hakuna jambo kama hilo kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo mitaani kudhibiti hali kama hiyo kama kuna ambao watakaidi kuelewa katazo lililotolewa Disemba 5,2025 kwa mujibu wa sheria za nchi.

Jeshi la Polisi Tanzania linaendelee kusisitiza kuwa, kinacho hamasishwa na kuitwa maandamano ya amani yasiyo na kikomo bado yamepigwa marufuku kwa sababu hayajafuata na wala hayaja kidhi matakwa ya Sheria Mama ambayo ni Katiba ya Mwaka 1977 pamoja na Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura 322.

Imetolewa na;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here