TMA yapongezwa kwa kuimarisha imani ya Watanzania kupitia taarifa sahihi za hali ya hewa

ARUSHA-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilipata fursa adhimu ya kutembelewa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa David Kihenzile(MB), katika Mkutano Mkuu wa 18 wa Tathmini ya Utendaji wa Sekta ya Uchukuzi. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa AICC jijini Arusha.
Katika mkutano huo, Mheshimiwa Naibu Waziri aliipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika utoaji wa taarifa sahihi na za kuaminika za hali ya hewa, ambazo zimeendelea kusaidia kuboresha usalama na ufanisi katika sekta ya uchukuzi na kuwa taasisi yenye kuaminiwa na Watanzania.

Mkutano huo unafanyika kwa muda wa siku tatu, kuanzia tarehe 15 hadi 17 Desemba,2025 na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya uchukuzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news