DAR-Leo Januari 16,2026 ni siku ya kuzaliwa kwa Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Hussein Mwinyi.
DIRAMAKINI, tunakupongeza kwa mchango wako mkubwa na wa mfano katika kuimarisha ustawi wa jamii, hususan kupitia jitihada zako za kuwakwamua wanawake, watoto na makundi yenye uhitaji maalumu nchini.
Uongozi wako wenye maono, huruma na uwajibikaji umeendelea kuwa chachu ya maendeleo na matumaini kwa wengi, ndani na nje ya Zanzibar.
Tunakuombea afya njema, hekima na mafanikio zaidi katika safari yako ya kuwatumikia wananchi na Taifa kwa ujumla.
Mwenyezi Mungu akujaalie wewe na mume wako, Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ali Mwinyi maisha marefu yenye baraka na awape nguvu ya kuendelea kutekeleza dhamira yenu njema ya kuwatumikia wananchi wa Zanzibar kwa ustawi bora wa kizazi cha sasa na kijacho.
Hongera na heri ya siku ya kuzaliwa, Mama Mariam Hussein Mwinyi.
Imetolewa leo Januari 16,2026 na,
Mtendaji na Mhariri wa DIRAMAKINI,

