WATU 10 wamefariki dunia na wengine 18 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia leo January Mosi 2026 katika eneo la Mwidu Mikese, mkoani Morogoro.
Ajali hiyo ilihusisha basi dogo na lori la mizigo imetokea katika Kijiji cha Maseyu, Kata ya Gwata, Wilaya ya Morogoro.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro ajali hiyo imetokea baada ya basi dogo lenye namba za usajili T 162 DMD, lililokuwa likiendeshwa na dereva aitwaye Sherehe Juma, kugongana na lori la mizigo aina ya HOWO lenye namba za usajili T 956 ELU na tela namba T 828 ELW.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















.jpg)