Mtu mmoja amefariki dunia huku wanne wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili kugongana uso jijini Tanga.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema ajali hiyo imetokea Machi 1, saa 6:10 usiku, katika eneo la Saruji, Wilaya ya Tanga, barabara Kuu ya Tanga-Segera.
Alisema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota Land Cruiser 'Ambulance' lenye namba za usajili STM 7202, mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, kugongana na gari la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T 628 DSG na T 637 DSG.
"Kutokana na ajali hiyo, mtu mmoja amepoteza maisha ambaye ni Zaharia Mdoe (41), mkazi wa Goha - Korogwe, aliyekuwa mgonjwa akisafirishwa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa ajili ya matibabu ya zaidi," amesema RPC Mchunguzi .
Aidha, aliwataja majeruhi kuwa ni Zainabu d Mdoe, Seleman Mdoe, Naiman Mdoe pamoja na Hatibu Hatibu, wote wakiwa abiria wa gari hilo la wagonjwa.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



.jpeg)




















