UDART yaendelea kupokea vipuri, kazi ya kufufua mabasi yaendelea saa 24

DAR-Kampuni ya Mabasi Yaendayo Kasi Jijini Dar es Salaam (UDART), katika kuendelea kuboresha huduma zake, imeendelea kuongeza mabasi zaidi katika mzunguko ili kuhakikisha wakazi wa Dar es Salaam wanapata huduma bora zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji wa UDART, Bw. Pius Ng’ingo, amesema kuwa, wanaendelea kupokea shehena kubwa ya vipuri, kutoka kwa watengenezaji wa mabasi hayo ya Golden Dragon, ya nchini China. 

Vipuri hivyo ndivyo vinavyotumika kuyafufua Mabasi yaliyokuwa yameharibika na kupaki kwenye karakana za UDART. Kwa vile mabasi yaliyokuwa yakifanya kazi yalikuwa machache, huduma ya usafiri huo ilizorota sana.

Hali hiyo ilimlazimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuteua safu mpya ya viongozi kuzisimamia DART na UDART, mnamo tarehe 2 Oktoba, 2025. 
Kasi ya ukarabati wa mabasi hayo na kuyaingiza barabarani kutoa huduma, iliongezeka, huku mafundi wakifanya kazi hiyo kwa shifti, usiku na mchana.

Hii ni habari njema ya mwaka mpya kwa wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam, wanaotegemea usafiri huu kwa shughuli zao za kiuchumi na kijamii.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, marehemu Ali Hassan Mwinyi naye mwaka 2016 aliacha msafara wake akapanda mabasi ya mwendo kasi.

Mkurugenzi Mkuu wa DART, Bw. Said Tunda alisema kuwa, Tanzania imekuwa nchi mfano barani Afrika na duniani kwa mfumo bora wa usafiri wa haraka mijini.

Bw. Tunda alisema kuwa Mataifa mengi yamekuwa yakija kujifunza kwa mwendokasi ya Tanzania, yakiwamo mataifa ya Singapore, Vietnam, Philipines, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, Senegal, Algeria, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na Wafanyakazi wa AU.

Serikali ya Marekani imekuwa ikileta mamia ya watu kutoka mataifa mbalimbali, kuja kujifunza hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here