Rais Dkt.Mwinyi azidisha uwekezaji katika Sekta ya Michezo Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa, Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuimarisha miundombinu ya viwanja vya michezo na akademia za michezo ili kuinua sekta ya hiyo nchini.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo Machi 20,2026, alipokutana na timu ya wataalamu wa masuala ya fedha kutoka Taasisi ya Tanzania Securities Limited, iliyoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Ndg. George Shumbusho, waliofika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameihakikishia taasisi hiyo kuwa, Serikali itashirikiana nayo ili wazo lao la kukuza mpira wa miguu, ikiwemo kuongeza thamani ya vilabu, kuboresha maslahi ya wachezaji na kuwajengea mazingira ya kutambua thamani yao linafanikiwa, kwani litatoa suluhisho la changamoto zilizopo katika sekta ya michezo.
Aidha, ameishauri Tanzania Securities Limited kuweka mkazo zaidi katika kuvijengea uwezo vilabu na vyama vya michezo katika masuala ya uongozi na uendeshaji, ili kuwa na mifumo madhubuti itakayowavutia wadau na wawekezaji kuvidhamini vilabu. Amebainisha kuwa kiini cha matatizo katika sekta ya michezo, hususan soka, ni ukosefu wa uongozi bora na uendeshaji.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Securities Limited, Ndg. George Shumbusho, amesema taasisi hiyo imejipanga vema kuhakikisha inaiongezea thamani Ligi Kuu ya Zanzibar, kuwa nyenzo muhimu ya kuitangaza Zanzibar kimataifa, pamoja na kuanzisha mfuko wa wawekezaji wenye lengo la kuongeza uwekezaji katika mpira wa miguu hapa nchini. 
Pia ameongeza kuwa watawajengea uelewa wa masuala ya fedha wachezaji ili kuwaandaa kwa maisha baada ya kustaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here