DAR-Waziri wa Fedha,Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, anayeziwakilisha pia nchi za Malawi,Zambia na Zimbabwe, Bw. Nathan Belete, Ofisini kwake katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadili kuhusu utekelezaji wa programu na miradi ya kiuchumi na kijamii inayofadhiliwa na benki hiyo.





