DAR-Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, Balozi Radhia Msuya ametoa ufafanuzi kuhusu idadi ya vifo iliyobainishwa katika ripoti ya tume hiyo.
Amesema, idadi hiyo imezingatia taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi kama vile Wizara ya Afya pamoja na ushahidi uliotolewa na mashuhuda waliojitokeza mbele ya tume wakati wa uchunguzi.
Balozi Msuya ameeleza kuwa,takwimu hizo zinawakilisha hali halisi hadi wakati tume inakamilisha uchunguzi wake, na kwamba zinaweza kubadilika endapo kutapatikana taarifa nyingine mpya na sahihi kutoka kwa mamlaka husika.
