Waajiri heshimuni Amri ya Serikali nyongeza ya mishahara-TUCTA

NJOMBE-Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya amewataka waajiri nchini kutekeleza amri ya nyongeza ya kima cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi kama inavyofanywa na Serikali.
Nyamhokya ametoa kauli hiyo Aprili 27, 2026 alipotembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano katika maonesho ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi yanayoendelea mkoani Njombe.

Alisema,Serikali ilitangaza kima hicho cha chini cha mishahara ambacho kimeanza kutumika mwezi Januari mwaka huu, ambapo hadi sasa takwimu zinaonesha ni takribani asilimia 80 tu ya waajili katika sekta binafsi wameanza kutekeleza.

“Nitoe wito kwa waajiri wa sekta binafsi nchini kutekeleza amri hii ya serikali kwa kuongeza mishahara husika... hatua itakayochangia ustawi na morali ya wafanyakazi,” amesisitiza Rais huyo wa TUCTA.

Akiwa katika banda hilo, Nyamhokya alipokea maelezo ya elimu zinazotolewa, ikiwemo elimu ya huduma za ajira, kinga ya jamii, sheria za kazi nchini pamoja na mahusiano baina ya Serikali na Makundi ya Kijamii yanayo jumuisha Taasisi za Dini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Wadau wa Siasa na Asasi za kiraia.

Alipongeza maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa elimu wanayoitoa kwa umma kwenye maonesho hayo, akisema inaakisi huduma za wizara kwa wananchi na wafanyakazi.

Pia, Nyamhokya amewahimiza wananchi na wafanyakazi kuendelea kutembelea banda hilo ili kupata elimu zaidi ikiwemo elimu ya kinga ya jamii.

Katika hatua nyingine, Rais wa TUCTA amewasihi wafanyakazi mkoani Njombe na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika sherehe za Mei Mosi zinazotarajiwa kufanyika kitaifa katika mkoa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here